THE BEST JOB BLOGGER IN TANZANIA, AFRICA

ADVERTISE YOUR JOB WITH US BY FOLLOWING OUR BLOG

Tuesday, November 16, 2010

MENEJA BIASHARA(BUSINESS MANAGER)

SIFA:
- Awe na Stashahada,shahada au sifa zinazofanana na hizo katika Nyanja ya biashara na utawala(Business and administration)
- Awe na uwezo wa kusimamia miradi ya biashara na mingineyo kwa ufanisi,hii ni pamoja na majukumu mengine ya Ofisi na kampuni.
- Awe na uelewa na mwenye uwezo wa kujifunza na kutekeleza masuala yanayohusiana na sheria/taratibu za uendeshaji wa kampuni.
- Awe na uwezo wa kutayarisha taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kampuni ambazo zitawasilishwa kwenye Bodi ya wakurugenzi kila baada ya miezi mitatu,hii ni pamoja na taarifa nyingine za utendaji za mara kwa mara.
- Awe na uwezo wa kuandaa ripoti za mauzo za siku,wiki na mwezi pia.
- Awe mwaminifu na kutumainiwa na mwenye msukumo binafsi(self driven)katika kutenda majukumu yake.Maana yake asiwe ni mtu wa kungojea kusukumwa na kukumbushwa majukumu yake ya kila siku.
- Awe ni mtu mwenye uwezo wa kupanga mipango yake inayoleta maslahi na maendeleo kwa kampuni na mwenye uwezo wa kuona mbali ili kupanua wigo wa kampuni.
- Atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa mwenyekiti mwendeshaji wa kampuni katika shughuli za utendaji za siku hadi siku.
- Awe na uwezo wa kutumia internet,Ms Excel,Ms Word,
- Atakuwa ndiye msimamizi wa uendeshaji wa Mini supermarket na restaurant ambazo zipo chini ya kampuni ya Ufishi consult ltd.
- Atakuwa ndiye msimamizi wa wafanyakazi wote wa kampuni na kusimamia taratibi zote za kampuni.
- Umri kati ya miaka 26-35

Tuma CV yako na barua ya maombi kwenye anuani ya kampuni hii ufishiconsult@gmail.com ,Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22/12/2010 na wale ambao watafanikiwa watapigiwa simu kwa ajili ya usaili